Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | French | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

MAHAKAMA YA AFRIKA IMEANDAA KONGAMANO ARUSHA KUADHIMISHA MIAKA 10

Na Kulwa Mayombi, EANA

Arusha, 19 Novemba, 2016 (EANA)-- Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu (AfCHPR) imeandaa kongamano la kimataifa jumatatu kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

Lengo la kongamano hilo, litakalofanyika kwa siku mbili jijini Arusha, yaliko makao makuu ya Mahakama,hiyo ni pamoja na kutathmini kazi za Mahakama hiyo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Kwa mujibu wa Rais wa Mahaka ya Afrika, Jaji Sylvain Ore,kongamano hilo litahudhuriwa na wajumbe 150 ambapo mwishoni mwa kongamano watatoa mapendekezo yatakayo kuza utendaji wa shughuli za mahakama katika siku zijazo.

Wajumbe wa kongamano hilo ni pamoja na wasomi ,taasisi za mashirika yasiyo ya kiserikali,tasisi za Umoja na Afrika (AU) na wawakilishi wa masuala ya sheria na wale wa taasisi za haki za binadamu kutoka ukanda wa Afrika .

Aidha kongamano hilo litafuatiwa na kikao cha ngazi ya juu cha Umoja wa Afrika kuhusu haki za Binadamu kitakacho fanyika November 23-26, pia jijini Arusha.

z
AfCHPR
 
 
 
 
 
 

Kikao hicho, ambacho kinatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kitapitisha mpango kazi wa miaka 10 kuhusu ukuzaji na ulinzi wa haki za Binadamu barani Afrika.

Mahakama ya Afrika ilianzishiwa mujibu wa kifungu namba Moja cha itifaki ya mkataba wa mahakama hiyo kwa lengo la kukamilisha na kuimarisha jukumu la kulinda haki za Tume ya Afrika ya Haki za Binadamuna Watu barani Afrika.

Hadi Octoba mwaka huu ni nchi 7 tu kati ya nchi 30 zilizoridhia itifaki , ndio zimetoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).

Nchi hizo 7 ni pamoja na Benin,Burkina Faso ,Cote d’lvoire,Ghana,Mali,Malawi naTanzania.

Aidha hadi Octoba mwaka huu, jumla ya maombi 119 ya mashauri yali pokelewa na mahakama hiyo na kesi 32 zimekamilishwa huku kesi 87 zikisubiri usikilizwaji.

MWISHO

 
Home...English News.. .Kiswahili News..French