Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | French | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

MAHAKAMA YA AFRIKA KUANZA KIKAO CHAKE JUMATATU ARUSHA NA KUSIKILIZA ZAIDI YA MASHAURI 50

Na Kulwa Mayombi, EANA

Arusha, 14 May, 2016 (EANA)--Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu (AfCHPR) inatarajia kuanza kusikiliza zaidi ya mashauri 50 Jumatatu May 16, katika kikao chake kitakachoanza jijini Arusha yaliyo makao makuu ya mahakama hiyo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari inasema kuwa mahakama hiyo itasikiliza mashauri hayo hadi Juni 03 mwaka huu.

Wingi wa mashauri yatakayosikilizwa mwaka huu umevunja rekodi ambapo mwezi Novemba mwaka 2014 mahakama hiyo ilisikiliza zaidi ya mashauri 20.

Wachunguzi wa mambo wanasema mashauri ya kusikilizwa na mahakama hiyo ya Afrika ya haki za binadamu na watu huenda yakaongezeka mara dufu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

AfCHPR
 
 
 
 
 
 

Mahakama hiyo ambayo mwaka huu inatimiza miaka 10 tangu ilipoanzishwa mwaka 2006 imekwisha toa hukumu 5.

Tayari Nchi 30 za umoja wa Afrika zimekwisharidhia mkataba ulioanzisha mahakama husika na kati ya hizo,nchi 8 ikiwemo Tanzania zimesaini tamko linaloruhusu mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na watu binafsi kupeleka mashauri moja kwa moja mbele ya mahakama hiyo.

Kwa sasa nchi za Afrika zinafanya msukumo wa kupanua majukumu ya mahakama hiyo ya Afrika ya haki za binadamu na watu kwa kujumuisha makosa ya jinai na hatimaye mahakama hiyo iitwe Mahakama ya Afrika ya haki na haki za binadamu chini ya itifaki ya MALABO ambayo hata hivyo imetiwa saini na nchi 8 tu hakuna nchi yoyote mwanachama wa umoja wa Afrika iliyoridhia itifaki hiyo.

Itifaki ya MALABO inaweza tu kufanya kazi endapo itaridhiwa angalau na Nchi 15.

KM/LC/MM/NI

 
Home...English News.. .Kiswahili News..French