Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | French | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

WANAHARAKATI ZAIDI YA 100 KUSHIRIKI KWENYE SEMINA YA MAHAKAMA YA AFRIKA NCHINI CHAD

Na Kulwa Mayombi, EANA

Arusha, 13 December, 2015 (EANA)--Zaidi ya wanaharakati 100, wanasheria , mashirika yasiyo za kiserikali na vyombo vya habari nchini Chad watakutana mjini N’djamena kwa siku mbili kuanzia 15-16 Desemba katika semina inayolenga kuitambulisha mahakama hiyo kwa wadau hao.

Semina hiyo inayoratibiwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu mkoani Arusha, itatanguliwa na semina nyingine ya siku moja ya uelemishaji zaidi juu ya shughuli za mahakama hiyo kwa waandishi waandamizi wa habari na wahariri wa nchini Chad itakayofanyika Jumatatu ( 14 Decemba).

Ujumbe wa Mahakama ya Afrika utaongozwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani.

AfCHPR
 
 
 
 
 
 

Kuanzia Desemba 2012 hadi sasa Mahakama hiyo ya Afrika imeendesha programu mbalimbali zenyelengo la kuitambulisha mahakama hiyo na tayari ziara 24, semina na mikutano 9 ya kikanda yenye lengo hilo la kuitambulisha mahakama imeshafanyika.

Lengo kuu la ziara hizo za uelemishaji ni kukuza na kulinda haki za binadamu barani Afrika ambapo lengo mahususi linajumuisha kukuza uelewa wa wananchi kuhusu Mahakama hiyo, kuzihamasisha Nchi za Afrika kuridhia na kutoa tamko kwa mujibu wa kifungu 34 (6) cha itifaki ya kukubali kuruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuleta kesi moja kwa moja mbele ya mahakama hiyo.

Uelemishaji huo ni kuhusu namna ya kufungua kesi katika mahakama hiyo na mwendo wa kesi na usikilizwaji wake, kuhamasisha wananchi kuhusu utatuzi wa migogoro inayohusu haki za binadamu.

Tangu kukubaliwa kwa itifaki ya kuanzisha mahakama hiyo mwaka 1998 ni nchi 29 tu kati ya nchi 54 wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ndizo zilizoridhia itifaki hiyo ambapo ni nchi saba tu ndizo zilizoridhia itifaki kukubali kuruhusu NGOs na watu binafsi kuleta kesi moja kwa moja mbele ya Mahakama ya Afrika.
Nchi hizo saba ni Burkina Faso, Mali, Ivory Coast,Ghana Rwanda, Malawi na Tanzania.

Mafanikio ya Mahakama hiyo kama chumbo cha kulinda haki za binadamu yanahitaji nchi nyingi zaidi wanachama kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo.

KM/LC/MM/NI

 
Home...English News.. .Kiswahili News..French