Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | French | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

CHUO KIKUU CHA KENYA CHASHINDA MASHINDANO YA MAHAKAMA YA MFANO

Na Kulwa Mayombi, EANA

Arusha, 9 Decemba, 2015 (EANA)--Chuo Kikuu Cha Moi ya Kenya kimeshinda mashindano ya majaribio ya mahakama (Moot Court Competition)a ya mfano baada ya kuvishinda vyuo vikuu kumi na moja vilivoingia fainali ya mashindano hayo.

Mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Arusha yaliratibiwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu mjini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo, Chuo hicho cha Moi kilipata ushindi wa asilimia 89.2. Chuo kikuu cha Zambia kilishika nafasi ya pili kwa karibu baada ya kupata alama ya asilimia 89.1 ambapo Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda kilipata ushindi wa alama ya asilimia 88.5 na kushika nafasi ya tatu.

Keny Map
 
 
 
 
 
 

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Augustino Ramadhani alisema washiriki 12 walioingia fainali katika mashindano hayo wameonyesha uelewa wa hali ya juu kuhusu mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika.

"Kutokana na matokeo yenu na ari mlionyesha tunaweza kusema kwamba mustakabali wa Afrika ni mzuri" alisema Jaji Duncan Tambala katika hotuba iliyosomwa kwa niaba ya Rais wa Mahakama hiyo na kuongeza kuwa Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu itaendelea kushirikiana na wanafunzi wa mafunzo ya sheria na vyuo vikuu vya Afrika kwa lengo la kukuza masuala ya Haki za Binadamu Barani Afrika.

Jaji mstaafu Ramadhani amevialika vyuo vikuu vya Afrika kushiriki mashindano ya Mahakama yatakayofanyika oktoba 21 2016 huko Banjul Nchini Gambia kama sehemu ya maadhimisho ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2016 ambao ni mwaka wa Haki za Binadamu mkazo ukiwa kuhusu haki za wanawake.

Waliongia fainali katika mashindano hayo mwaka huu ni pamoja na Chuo kikuu cha katoliki cha Afrika ya Kati kilichopo Cameroon, Chuo Kikuu cha Makerere cha Nchini Uganda, Chuo kikuu cha Moi cha Nchini Kenya, Chuo kikuu cha Pretoria cha Afrika ya Kusini, Chuo kikuu cha Zambia, Chuo cha Burkina Faso na Chuo kikuu cha ibadan cha Nchini Nigera.

Vyuo vingine ni Chuo kikuu cha Zimbabwe, Chuo kikuu cha Nigeria, Chuo kikuu cha Nsukka cha Nchini Nigeria, Chuo kikuu cha St. Augustine cha Nchini Tanzania, Kituo cha maendeleo ya sheria cha Nchin Uganda na Chuo cha Haramaya cha Nchini Ethiopia.

Kila Nchi iliwakilishwa na wanafunzi wawili pamoja na mkufunzi wao.

Mashindano ya Mahakama ya Mfano yaliandaliwa kwa pamoja na Mahakama ya Afrika na mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na watu (AfCHPR), kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Kamati ya wataalamu ya masuala ya haki na ustawi wa mtoto pamoja na kufadhiliwa na shirika la misaada ya maendeleo la Ujerumani (GIZ)

Madhumuni ya mashindano hayo ya mahakama ya mfano yalikuwa ni kuwaelemisha viongozi watarajiwa kuhusu mfumo wa haki za binadamu wa Afrika , masuala ya utawala, kuunda mitandao baina ya taasisi za Afrika za elimu ya juu zinazopendelea kujifunza masuala mbalimbali na kazi za umoja wa Afrika.

KM/LC/MM/NI

 
Home...English News.. .Kiswahili News..French