Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | French | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

MAHAKAMA YA AFRIKA YAHAMASISHA WALESOTHE

Na Mtua Salira,EANA


Arusha, Julai 7,2015 (EANA) – Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR) inafanya ziara ya siku mbili nchini Lesotho kwa lengo la kuishiwa nchi hiyo kuhamasisha kazi za mahakama hiyo nchini humo.

Kazi hiyo inayofanyika kati ya Julai 6 na 7, mwaka huu, pamoja na mambo mengine itatembelea maofisa wa ufalme huo wakiwemo Waziri Mkuu, mawaziri wa Mambo ya Nje na Sheria pamoja na Rais wa Baraza la Seneti.

Katika ratiba yake AfCHPR pia itaendesha semina juu ya haki za binadamu katika Ufalme huo itakayofanyika katika Hoteli ya Sun Maseru, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwa Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA).

Ujumbe wa Mahakama katika kazi hiyo unajumuisha majaji watatu na msajili.

AfCHPR
 
 
 
 
 
 
Kuanzia mwaka 2010 Mahakama hiyo imekuwa ikifanya kampeni ya kuhamasisha programu zake katika nchi mbalimbali ambapo mpaka sasa imeshafanya ziara za uhamasishaji 22 pamoja na semina na mikutano ya kanda na ya kibara tisa.

Tangu kuanzishwa kwa itafaki ya mahakama hiyo zaidi ya miaka 16 iliyopita nchi 28 kati ya nchi 54 wanachama Umoja wa Afrika (AU) zimesharidhia.

MS/LC/MM/NI
 
Home...English News.. .Kiswahili News..French