Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

31.03.12 - EAC/ZIWA VICTORIATO - EAC KUPATA DOLA ZAIDI YA MILIONI 7 KWA AJILI YA MIRADI ZIWA VICTORIA

Na James Gashumba,EANA

Arusha, Machi 31, 2012(EANA) – Nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinatarajiwa kupokea kiasi cha dola za Kimarekani milioni 7.3 kwa ajili ya shughuli za uhifadhi wa mazingira ya ziwa Victoria kutoka Benki ya Dunia, afisa mmoja wa EAC amesema.

awamu ya Pili(LVEMP II), ambao unalenga kuboresha ushirikiano wa uhifadhi wa Bonde la ziwa Vicotria kupunguza uharibifu wa mazingira kama vile uchafuzi wa maji na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Fedha hizo ziliidhinishwa katika mkutano uliofanyika hivi karibuni mjini Kigali, Rwanda ambao ni wa tano wa kamati ya kanda ya mradi huo wa LVEP II. Fedha hizo zitatumika katika shughuli za uhifadhi wa mazingira ya kanda katika kipindi cha mwaka wa fedha cha 2012-2013.

Fedha hizo zitatumika katika mpango wa maendeleo ya matumizi bora ya rasilimali maji katika ziwa Victoria, kusimamia mfumo wa taarifa za rasilimali maji yanayoonekana, yaliyopo ardhini na ubora wake.

Kamati ya usimamizi ya mradi huo pia imepokea taarifa mbalimbali za ushauri ikiwa ni pamoja na ile ya Mkakati wa Usimamizi endelevu wa ardhi ya Bonde,mapendekezo ya kuoanisha viwango vya sumu ya maji yanayotoka kwenye viwanda na manispaa na kumwagwa katika Bonde la ziwa Victoria na Mkakati wa udhibiti na usimamizi wa magugu maji katika ziwa Victoria.

‘’Lengo la mradi huo ni kuboresha ushirikiano na kuweka rasilimali hiyo asilia ya Bonde la ziwa Victoria katika hali nzuri yenye kufaa kwa uzalishaji,’’ alisema Charles-Martin Jjuuko, Mfisa Mawasiliano na Uhamasishaji wa Tume ya Ziwa Victoria.

Kwa mujibu wa Dk. Roze Mukankomeje,Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Mazingira wa Rwanda(REMA),kiasi cha dola za Kimarekani milioni 15, ambao ni mgao wa Rwanda, zitatumika katika uhifadhi wa vyanzo vya maji, ikiwa ni pamoja na kurejesha maeneo oevu na uoto wa asili.

JG/FJ/NI