Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

21.03.12 - EAC/UCHUNGUZI - MTAALAMU WA EAC ASEMA KITUO CHA UCHUNGUZI KITAPUNGUZA UHALIFU

Na Mark Mugisha, EANA

Arusha, Machi 21, 2012 (EANA) – Mkuu wa Kitengo cha Amani na Usalama katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Didacus Kaguta amelezea matumaini yake kwamba Kituo cha Uchunguzi cha Rufaa cha Kanda kwa Masuala ya Uhalifu (RRFC) kinachotarajiwa kuanzishwa, kitaweza kusaidia kupunguza uhalifu ndani ya kanda.

Kaguta alitoa maoini hayo Jumanne wiki hii alipokuwa anawahutubia wataalamu wa uchunguzi wa masuala ya uhalifu kutoka nchi wananchama wa EAC, makao makuu ya jeshi la Polisi, mjini Kampala, Uganda.

‘’Kituo kitachangia katika kupunguza uhalifu kwa sababu moja kati ya vipengele vyake ni kuweka viwango sawa kwa maana ya kuoanisha taratibu za huduma za kufanyia uchunguzi uhalifu katika kanda,’’ Kaguta aliliambia Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA).

Wataalumu hao wamekuwepo nchini Uganda katika juhudi zao za kutafuta mahali muafaka pa kujenga kituo hicho cha RRFC.

Kaguta alisema wataalamu wote wa idara ya uchunguzi wa masuala ya uhalifu katika nchi wananchama watakuwa wanakuta mara kwa mara.

‘’Tunachokiingalia hivi sasa ni kiasi gani serikali za nchi wanachama zimeingiza katika miundombinu ya idara hizi na nini kinahitajika iwapo eneo la ujenzi wa kituo hicho cha kanda litapatikana.’’ alisema.

Grace Akullu, Mkurugenzi wa Idara ya Makosa ya Jinai wa Uganda, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo, Luteni Jenerali Kale Kayihura, alirudia utayari wa nchi yake kupokea ujenzi wa kituo hicho.

Alisema kuwepo au kutokuwepo ufadhili wa fedha kutoka nje, serikali yake iko tayari kuipatia idara ya uchunguzi vifaa na mipango iko mbioni kuipandisha hadhi idara hiyo kuwa kurugenzi.

“’Idara ya Uchunguzi wa masuala ya uhalifu inashirikishwa ndani ya idara ya makosa ya jinai na ipo haja ya kuikuza na tupo katika mchakato wa kupata machine ya kisasa ya kuchunguza alama za vidole na kuwa na benki ya takwimu,’’ alisema.

Kesi nyingii katika nchi wananchama hutupiliwa mbali na mahakama kutokana na kukosekana kwa vidhibiti vilivyofanyiwa uchunguzi wa uhakika ili kuunga mkono mashitaka.

NI/MM/LC