Home... |... EANA... | ...English News... | ...Kiswahili News... | ....Archives. ... |... ..Audio.. | ... Photo Gallery
 

04.03.12 - WAPITISHA AZIMIO LA KUUNDA BARAZA LA WAZEE WA BUSARA EAC

Na Dennis Bizimana, EANA

Arusha, Machi 04, 2012 (EANA) – Wataalamu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamepitisha azimio la kuanzisha Baraza la Wazee wa Busara EAC kwa ajili ya kuzuia na kutoasuluhisho la amani la migogoro ndani ya kanda.

Wataalamu hao waliidhinisha namna Baraza hilo litakavyofanya kazi zake katika kikao chao kilichofanyika mjini Bujumbura, nchini Burundi hivi karibuni, linaripoti Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA).

Baraza hilo la Wazee litatoa maelekeza kwa kanda kuhusu kuendesha diplomasia ya kuzuia migogoro na kutafuta suluhisho muafaka pindi inapotokea.

Ms Kiraso
 
 
 
 
 
 

Baadhi ya migogoro iliyomo kwenye vichwa vya wataalumu hao ni pamoja na ule wa hivi karibuni unaohusiana na ghasia baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, mgogoro wa visiwa vya Migingo, ghasia za Zanzibar kabla na baada ya uchaguzi na ghasia nchini Uganda, baada ya uchaguzi mkuu.

‘’Tunahitaji viongozi wenye busara na kuheshimika na wasiopendelea yeyote (wanaume kwa wanawake) kutoka nchi wananchama wa EAC ambao wanaweza kuingilia kati kuzima mambo kabla ya kufikia katika hatua ya mgogoro kamili,’’ afisa mmoja aliyehudhuria mkutano huo aliieleza EANA.

Kwa mujibu wa vifungo vya Mswada wa Awali, Baraza hilo limepewamamlaka ya kutoa ushauri kwa mkutano w a wakuu wa nchi, baraza la mawaziri na katibu mkuu wa EAC katika masuala yote yanayohusiana na kukuza na kulinda amani,usalama na utulivu katika jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kukuza na kulinda pia haki za binadamu , heshima kwa utawala wa sheria na pia masuala muhimu ya kuelekea katika mtangamano wa shirikisho la kisiasa.

‘’Baraza linaweza, kama linaona kuna umuhimu, na pia katika haliambayo linafikiri inafaa, kujitangazia lenyewe juu ya suala lolote linalohusiana na kukuza na kulinda amani, usalama na utulivu Afrika Mashariki na mambo mengine yanayohusiana nayo,’’ inasomeka sehemu ya mswada huo wenye kurasa 12.

Baraza hilo litakuwa na mjumbe mmoja kutoka kila nchi mwanachama wa EAC, mwenye kuheshimika sana na huru, mwenye hadhi na ambaye amewahi kutoa mchango wa pekee katika masuala yanayohusu amani, usalama na maendeleo katika ngaza za kitaifa, kikanda, bara na kimataifa.

Wajumbe hao pia hawatakiwi kushika wadhifa wowote wa kisiasa mudawanapoteuliwa kutumikia Baraza hilo.

Mapema, Naibu Katibu Mkuu wa EAC, anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Beatrice Kiraso alisema Baraza hilo la Wazee, litaipatia kanda hiyo, uwezo wa kuendeesha diplomasia ya kuzuia uwezekano wa
kutokea migogoro itakayoweza kuleta ghasia katika hatua za awali na kama ikiwa imeshatokea basi litaweza kuidhibiti na kuimaliza kwaamani.

Mswada wa Baraza hilo utawasilishwa mbele ya Baraza la Pamoja la Kisekta juu ya Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi, Usalama baina ya nchi na Uratibu wa Sera ya Mambo ya Nje kwa ajili ya kufikiriwa na
kupitishwa kabla ya kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri.

NI/LC